WHO yaitaka serikali ya Ethiopia na wenzi wake kuongeza juhudi dhidi ya mlipuko unaoendelea wa kipindupinduTaasisi za fedha za kimataifa zaongeza makadirio ya uchumi wa China kwa mwaka 2023
2023-10-19 14:42:56| cri

Taasisi za fedha za kimataifa zimeongeza makadirio yao ya ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka 2023 baada ya uchumi wa nchi hiyo kuongezeka kwa kasi kuliko ilivyotarajiwa katika robo ya tatu ya mwaka huu.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa, Kundi la Citigroup linatarajia pato la ndani la China kukua kwa asilimia 5.3 kutoka asilimia 5 ya awali.

Kampuni ya JP Morgan imekadiria uchumi wa China utakua kwa asilimia 5.2 mwaka huu, ikiwa ni Zaidi ya makadirio ya asilimia 5, huku kampuni ya Morgan Stanley ikiongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kwa asilimia 5.1 kutoka asilimia 4.8 mpaka 4.9 ya awali.

Benki ya UBS ya nchini Uswisi imeongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China mpaka asilimia 5.2, ikiwa ni alama 0.4 zaidi ya makadirio ya awali.