Waziri wa Mambo ya Nje wa China asifu mafanikio ya mkutano wa tatu wa BRF
2023-10-19 14:42:26| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, amesema Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, umeashiria hatua nyingine kubwa katika mchakato wa kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kusema mkutano huo umefanyika kwa mafanikio.

Wang Yi amesema maafikiano muhimu yaliyofikiwa katika mkutano huo ni kufungua ngazi mpya ya ubora wa juu wa ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kuongeza kuwa, ngazi mpya ya ushirikiano itatoa fursa zaidi mpya kwa uchumi wa dunia na kuwa na manufaa kwa hali ya sasa ya dunia.

Amesema Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limetoa fursa ya jukwaa la ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya pamoja na kusaidia nchi nyingi zinazoendelea kuongeza kasi ya mchakato wa kuwa nchi za kisasa.