China yasikitishwa na kutopitishwa kwa azimio linalohusu suala la Israel na Palestina katika Baraza la Usalama la UM
2023-10-19 09:21:33| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ameeleza masikitiko yake kufuatia Baraza la Usalama la umoja huo kushindwa kupitisha azimio linalohusu mgogoro kati ya Israel na Palestina.

Muswada wa azimio hilo ulioandaliwa na Brazil ulipata kura 12 za ndio kwenye Baraza la Usalama, lakini ulishindwa kupitishwa kutokana na Marekani kuupigia kura ya turufu.

Akiongea baada ya upigaji kura wa azimio hilo, Balozi Zhang Jun amesema China inasikitishwa na kutopitishwa kwa azimio hilo. Hata hivyo kutokana na hali ya ukanda wa Gaza kuzorota haraka, ambapo shambulio la anga la Oktoba 17 dhidi ya hospitali limesababisha vifo vya mamia ya raia, Balozi Zhang Jun amelitaka Baraza la Usalama lichukue hatua za haraka na zenye nguvu.