Rais wa Jamhuri ya Kongo asema BRI ni muhimu kwa maendeleo ya Afrika
2023-10-19 09:30:39| CRI

Rais Denis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Kongo amesema pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limeingiza raslimali muhimu katika maendeleo ya Afrika.

Akiongea kwenye Baraza la ngazi ya juu la Uchumi wa Kidijitali chini ya Kongamano la tatu la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Rais Sassou Nguesso amesema utekelezaji wa BRI umeboresha kwa kiasi kikubwa miundombinu katika bara la Afrika na kuhimiza ujenzi wa eneo huru la biashara la bara la Afrika.

Amefahamisha kuwa miradi yote ya ushirikiano chini ya BRI ikiwemo ya ujenzi ya reli, barabara na miundombinu ya maji, mashine za kilimo na uwekaji wa kebo, ni muhimu kwa maendeleo ya Afrika na itasaidia Umoja wa Afrika kutimiza malengo yake ya Ajenda 2063.