Waziri wa ulinzi wa Israel awaambia askari kujiandaa kwa mashambulio ya ardhini dhidi ya Gaza
2023-10-20 11:31:48| cri

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amewataka askari wa miguu katika eneo la mpaka na Ukanda wa Gaza kujiandaa kuingia Palestina, lakini hakutaja muda halisi wa uvamizi huo.

Gallant alitembelea Kamandi ya Kusini ya Israel iliyo karibu na Gaza, ambako Israel imekuwa ikikusanya wanajeshi wake baada ya shambulio la ghafla lililofanya na wapiganaji wa kundi la Hamas Oktoba 7 mwaka huu.

Jana jioni, jeshi la Israel lilitoa taarifa ikisema, kama sehemu ya kukamilisha maandalizi ya kuendelea na mapigano, kibali cha mipango ya operesheni na kupelekwa kwa askari katika uwanja wa vita vinaendelea.

Taarifa hiyo imesema, Afisa wa Kamandi ya Kusini Yaron Finkleman ametembelea vikosi mbalimbali vilivyoko katika eneo la kusini na kuridhia mipango ya mashambulio.