Rais Xi Jinping wa China akutana na rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso
2023-10-20 09:40:40| CRI

Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso aliyekuja China kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Baraza la tatu la Ushirikiano wa Kimataifa la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Rais Xi amesema Jamhuri ya Kongo ni mwenzi na mshirika muhimu kwenye ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Amesema ushirikiano wa pande mbili umepata matokeo mazuri, na utekelezaji wa miradi mbalimbali umefanikiwa ikiwemo mradi wa Barabara Kuu No.1 ya Taifa la Kongo. Rais Xi amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana kwa karibu na Jamhuri ya Kongo ili kuhimiza ujenzi wa utaratibu wa kimataifa ulio wa haki na halali.

Rais Sassou Nguesso amesema ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ni mradi mkubwa unaotoa mfumo mpya wa maendeleo jumuishi. Kufanyika kwa mafanikio Mkutano wa Kilele wa Baraza la tatu la Ushirikiano wa Kimataifa la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kumeonesha uungaji mkono thabiti wa nchi washiriki, ikiwemo Jamhuri ya Kongo.