EAC yazindua taasisi ya kusimamia vyombo vya habari vya kikanda
2023-10-20 11:31:21| cri

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana alhamis imezindua Baraza la Habari la Afrika Mashariki (EAPC) litakalokutanisha mamlaka za kusimamia vyombo vya habari ndani ya kanda hiyo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana, EAC imesema Baraza hilo lililozinduliwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Peter Mathuki jijini Arusha, Tanzania, lina wajumbe kutoka vyombo vya habari na mabaraza ya wanahabari katika nchi wanachama wa EAC, kwa lengo la kuboresha na kulinda uhuru, taaluma na uwajibikaji wa vyombo vya habari katika kanda hiyo.

Amesema ni muhimu kwa tasnia ya habari, kama mdai wa maingiliano ya watu kuanzia ngazi ya mashinani, kuelewa kikamilifu mchakato husika ili kuwafahamisha watu wao kwa lugha rahisi inayoeleweka kwao, na kuongeza kuwa kuviwezesha vyombo vya habari katika masuala ya maingiliano ni ufunguo muhimu sana.