Kenya yatangaza mpango wa kuhifadhi misitu
2023-10-20 09:02:27| CRI

Kenya imetangaza mpango wa kuweka mipaka ya misitu yote nchini humo na kuweka uzio kwenye mipaka hiyo ili kuzuia uvamizi wa binadamu na shughuli nyingine haramu.

Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu wa Kenya Soipan Tuya amesema kupitia taarifa kuwa shughuli kadhaa zinazoharibu misitu, ikiwemo ukataji haramu wa miti na uchomaji wa mkaa, zimeendelea kwa muda mrefu, na serikali inadhamiria kuzikomesha.

Waziri huyo amesema, operesheni inayoshirikisha idara husika dhidi ya uhalifu wa misitu itafanyika katika maeneo yote ya misitu nchini Kenya.

Serikali ya Kenya inaendelea na kampeni ya kupanda miti bilioni 15 ndani ya miaka kumi ili kuongeza misitu na kuikinga nchi hiyo dhidi ya athari hasi za mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo maafa ya ukame.