Huawei yaingia makubaliano ya kufanya sekta za serikali, usafiri na elimu kuwa za kidijitali nchini Kenya
2023-10-20 11:30:53| cri

Serikali ya Kenya imeshirikiana na kampuni ya teknolojia ya China, Huawei, kuboresha miundo mbinu ya kidijitali na kufanya sekta za serikalii, usafiri na elimu kuwa za kidijitali.

Rais William Ruto Jumatatu alishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya maelewano (MoU) kati ya serikali na Huawei mjini Beijing, China, ambapo aliiona kampuni hiyo kama "mshirika wa kutegemewa" katika kuboresha miundombinu ya kidijitali ya Kenya.

Mwenyekiti wa Huawei Liang Hua alisema kampuni hiyo iko tayari kufanya kazi kwa karibu zaidi na serikali ya Kenya ili kukuza uchumi wa kidijitali na kiubunifu nchini humo.