Uganda, Kenya na Tanzania kupata fedha kwa ajili ya kutengeneza chanjo ya VVU
2023-10-20 11:29:12| cri

Uganda, Kenya na Tanzania ni miongoni mwa nchi nane zilizopokea fedha kutoka Shirika la Misaada la Marekani (USAid) kiasi cha dola milioni 45 kwa ajili ya kutafiti na kutengeneza chanjo ya VVU/UKIMWI, kutokana na kuwepo mapungufu ya ufadhili katika kuendeleza dawa na chanjo jambo ambalo limezilazimisha nchi za Afrika kutegemea vifaa vya wafadhili wa dawa.

Nchi nyingine zilizopata ufadhili huo ni pamoja na Zambia, Nigeria, Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji.

"Lengo letu ni kupata chanjo ambayo itazuia maambukizi ya VVU kwa ufanisi wa asilimia 60 au 80," alisema Dk Cissy Kityo, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Kliniki ya Pamoja cha Uganda (JCRC).