China yaihimiza jumuiya ya kimataifa kusaidia Somalia kukabiliana na changamoto
2023-10-20 09:37:16| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Somalia kukabiliana na changamoto.

Akiongea kwenye mjadala kuhusu suala la Somalia kwenye Baraza la Usalama la umoja huo, Balozi Dai amesema hivi sasa, wakati mchakato wa usalama na siasa wa Somalia uko katika kipindi muhimu, ufuatiliaji na uungaji mkono wa Jumuiya ya Kimataifa hauwezi kulegezwa, ili kuisaidia Somalia kukabiliana na changamoto, na juhudi za kupambana na ugaidi zinatakiwa kuimarishwa.

Pia amesema mchakato wa mpito wa kisiasa wa Somalia unatakiwa kuungwa mkono. China inaunga mkono pande mbalimbali za Somalia kufanya mazungumzo ya kitaifa, kuhimiza mazungumzo ya kisiasa na kujadili masuala ya uchaguzi, mapambano dhidi ya ugaidi na makubaliano ya amani.