Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Msumbiji
2023-10-20 09:38:06| CRI

Rais Xi Jinping wa China amekutana na waziri mkuu wa Msumbiji Bw. Adriano Maleiane ambaye yuko ziarani nchini China kuhudhuria mkutano wa 3 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Rais Xi amepongeza ushirikiano kati ya China na Msumbiji na maendeleo yaliyopatikana katika ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika ikiwemo Msumbiji kujenga “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kuhimiza uungaji mkono wa utekelezaji wa hatua tatu za ushirikiano, likiwemo pendekezo la maendeleo ya viwanda la Afrika, mpango wa China kusaidia maendeleo ya kilimo ya Afrika, na mpango wa ushirikiano wa kuandaa watu wenye ujuzi kati ya China na Afrika.

Bw. Maleiane amesema, anafurahia kuhudhuria mkutano wa 3 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na ziara yake imeimarisha ufahamu wake kuhusu China na pendekezo la “Ukanda Mmoja,  Njia Moja”, na kuzidi kufahamu mtazamo wa mbali na wa kimkakati ya rais Xi. Mapendekezo muhimu likiwemo pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na pendekezo la maendeleo ya dunia yanasaidia nchi nyingi kuondokana umaskini, kupata maendeleo ya kiuchumi na kuboresha maisha ya watu.