Huduma za matibabu za China zawanufaisha Watanzania milioni 20
2023-10-20 22:29:40| cri

Takriban Watanzania milioni 20 wamenufaika na huduma za kitaalamu za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wa China ambao wamekuwa wakifanya kazi kwenye kambi mbalimbali za matibabu nchini Tanzania kwa takriban miaka 60 sasa.

Balozi wa China nchini Tanzania, Bibi Chen Mingjian alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kambi ya madaktari bingwa katika wilaya ya Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma, ambapo madaktari bingwa 11 kutoka China watatoa huduma ya ushauri na upasuaji kwa watu wa eneo hilo kwa muda wa siku tano.

Balozi Chen alisema kambi hizo za madaktari ni sehemu ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulioanzishwa na waasisi wa mataifa hayo mawili, ambapo mwaka 1964 na 1968, China ilianza kupeleka timu za madaktari Zanzibar na Tanzania Bara.