Wanasayansi wawili wa Uganda washinda Tuzo ya Africa Young Innovators for Health
2023-10-21 22:42:22| cri

Wanasayansi wawili wa Uganda, waliopokea Tuzo ya Wavumbuzi Vijana wa Afrika kwa Afya kwa ajili ya michango ya Huduma ya Afya kwa Wote, wameahidi kutumia heshima hiyo kuongeza kazi zao na kuleta matokeo kwa ajili ya nchi yao na bara la Afrika.

Katika mahojiano tofauti na Monitor, Dkt Ochora Moses, mshindi wa tuzo ya kwanza, na Bi Izath Nura, mshindi wa pili, walisema tuzo zao zimebadilisha maisha yao. Wawili hao wa Uganda walitunukiwa pamoja na Wanigeria wawili, huku Bi Teniola Aderonke Adedeji akiwa mshindi wa kwanza na Bw Abdullahi Muhammad Habibu akiwa mshindi wa pili.

Tangazo hilo lilitolewa katika kongamano la ‘Galien Africa’, ambalo linaadhimisha ubunifu na ubora katika sayansi barani Afrika.