Kampuni ya uhandisi ya China yasifiwa kwa kuipandisha daraja la juu Zanzibar
2023-10-23 09:44:40| CRI

Mamlaka ya visiwa vya Zanzibar, Tanzania imeipongeza Kampuni ya Jianchang ya Uhandisi wa Reli ya China (CRJE) katika Afrika Mashariki kwa kuipandisha juu Zanzibar na kuifanya kuwa katika nafasi mpya.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika Jumamosi ya kuadhimisha miaka 20 ya kampuni hiyo visiwani Zanzibar, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, alisema katika miongo miwili iliyopita, CRJE imefanikiwa kukamilisha miradi 35 visiwani Zanzibar, ikiwemo hoteli, shule, hospitali, majengo ya ofisi na miradi mingine ya miundombinu.

Waziri Mazrui ameipongeza CRJE wakati inapoelekea kujenga mustakabali mzuri kwa Zanzibar, akibainisha kuwa Serikali ya Zanzibar inawakaribisha wawekezaji wengine kuwekeza katika visiwa vya Zanzibar baada ya CRJE kuonesha utendaji kazi wa hali ya juu katika miradi yake katika hali ya kunufaishana.

Kwa upande wake Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Zhang Zhisheng alisema CRJE ni kampuni inayomilikiwa na serikali ya China ambayo imetekeleza miradi mingi nchini China na duniani kote ikiwemo Tanzania bara na Zanzibar na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya China na nchi nyingine.