Mtaalamu wa Marekani asema pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” linainufaisha dunia nzima
2023-10-23 09:37:11| CRI

Mtaalamu wa Marekani anayeshughulikia suala la Afrika Lawrence Freeman alipohijiwa hivi karibuni alisema pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” linatoa mchango muhimu katika kuboresha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi duniani, na linainufaisha dunia nzima.

Alisema ukosefu mkubwa wa umeme ni suala kubwa zaidi kwenye sekta ya miundombinu huko Afrika, China inashirikiana na nchi nyingi za Afrika kutatua suala hilo. Miradi ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja” barani Afrika imehusisha sekta za nishati, bandari, uwanja wa ndege, barabara, reli, shule na nyinginezo, na kwamba suala la China haina mbadala kwa ushiriki wake kwenye ujenzi wa miundombinu na maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika limekuwa hali halisi isiyokanushwa.

Akizungumzia kuhusu shutuma zisizo na msingi zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wa Marekani juu ya pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Freeman amesema China haitaingilia kamwe mambo ya ndani ya nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo hilo, hakuna sharti linaloongezwa kwenye mkopo wa miradi ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Kitendo cha baadhi ya wanadiplomasia na wabunge wa Marekani kukashfu sera ya China kwa Afrika bila ya msingi wowote kinalenga kueneza habari za uongo kwa makusudi.