Maofisa na wataalamu watoa wito wa kuanzisha ushirikiano wa China na Ethiopia katika ufundi stadi
2023-10-23 23:54:33| cri

Wataalamu na watunga sera wanaohudhuria semina ya ngazi ya juu kuhusu uratibu wa China na Afrika katika elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) wametoa wito wa kuimarisha uhusiano wa China na Ethiopia katika mafunzo hayo.

Semina hiyo ilifanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, na kuhudhuriwa na maofisa wa ngazi ya juu wa Ethiopia na maofisa wa China, wasomi na wataalamu.

Waziri wa Kazi na Ujuzi wa Ethiopia, Teshale Berecha amesisitiza kuwa kuna haja kubwa ya kuendeleza mafunzo na uratibu kati ya China na Ethiopia katika eneo la ufundi na mafunzo ya ufundi stadi. Amesema uratibu kati ya nchi hizo mbili katika eneo hilo si kwamba ni sehemu ya elimu, bali pia ni daraja linalounganisha mataifa hayo mawili, kuimarisha kuelewana, na kuongeza nguvu ya uhusiano wa pande hizo.

Kwa upande wake, mkurugenzi mkuu wa Ushirikiano wa Elimu ya Ufundi Stadi kati ya China na Afrika, Gong Zhiwu, amesema ushirikiano huo umezindua miradi mbalimbali katika nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Ethiopia, Tanzania, Rwanda, Kenya, Uganda na Visiwa vya Shelisheli.