Rais wa Tanzania asema mkataba bandari unaenda kuongeza mapato
2023-10-23 10:55:35| cri

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema mikataba iliyoingiwa kati Serikali na kampuni ya DP World ya mjini Dubai, inaenda kuongeza mapato ya serikali, hivyo kukuza uchumi wa taifa.

Amesema bandari ya Dar es Salaam ni lango la biashara kwa nchi zinazozunguka, hivyo ni wajibu kuwekeza, kuboresha na kuhudumia nchi zinazoizungukaTanzania kama nyenzo ya kiuchumi pia kwa kuzingatia mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN), unazozitaka nchi za mlango bahari kuhudumia nchi nyingine.

Rais Samia amesema hayo jana jumapili, Ikulu ya Chamwino, Dodoma katika hafla ya utiaji saini wa mikataba mitatu ya uendelezaji na uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, kati ya Serikali ya Tanzania chini ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na Kampuni ya DP World ya mjini Dubai.