China yaitaka Ufilipino kuacha kuzusha machafuko na kufanya uchochezi baharini
2023-10-23 09:46:01| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameitaka Ufilipino kuacha kuzusha machafuko na kufanya uchochezi baharini ikiwa ni pamoja na kuacha kufanya mambo ya hatari.

Hayo aliyasema alipozungumzia tukio la hivi karibuni katika Bahari ya Kusini ya China. Siku ya Jumapili, Ufilipino ilipeleka vifaa kinyume cha sheria kwenye meli ya kivita "iliyotia nanga" huko Ren'ai Jiao. Walinzi wa Pwani ya China (CCG), kwa mujibu wa sheria, walizuia meli za Ufilipino ambazo ziliwasilisha vifaa vya ujenzi kinyume cha sheria.

Msemaji wa China amebainisha kuwa meli mbili za kiraia na meli mbili za walinzi wa pwani za Ufilipino zilivamia maji ya Ren'ai Jiao huko visiwa vya Nansha, China Oktoba 22 bila ya idhini ya China. Zikipuuza onyo lililotolewa mara nyingi na meli za CCG, meli za Ufilipino zilikwenda moja kwa moja hadi rasi ya Ren'ai Jiao na kugongana vibaya na meli za CCG zinazotekeleza sheria kwenye eneo la tukio na meli za uvuvi za China zilizokuwa kwenye shughuli za kawaida za uvuvi.

Msemaji huyo alisisitiza kuwa Ren'ai Jiao ni sehemu ya visiwa vya Nansha vya China na ni eneo la China. Ufilipino iliweka meli yake ya kivita kinyume cha sheria katika eneo hilo, na kukiuka kwa kiasi kikubwa mamlaka ya eneo la China.