Tarehe 18 Oktoba ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kukoma Hedhi, ama Menopause kwa lugha ya kiingereza. Wakati mwanamke anapokaribia kukoma hedhi, kuna mambo mengi yanajitokeza katika mwili wake, na kama hatapata huduma inayostahili, anaweza kujikuta akiwa na wakati mgumu sana. Umri wa kukoma hedhi unategemea na mwanamke husika, kuna wengine wanakoma hedhi wakiwa na miaka ya 40, wengine miaka ya 50 na kuendelea. Lakini kuna sababu nyingine ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kukoma hedhi mapema zaidi, ambazo ni pamoja na magonjwa kama saratani, unene uliopitiliza, na kula aina fulani ya vyakula kwa wingi.
Katika kipindi cha leo cha Ukumbi wa Wanawake, tunaangalia suala zima la kukoma kwa hedhi.