CMG na kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Paris wasaini Hati ya Kumbukumbu ya Ushirikiano
2023-10-24 10:42:35| cri

Mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Shen Haixiong na mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Paris Bw. Tony Estanguet jana Oktoba 23 walitia saini Hati ya Kumbukumbu ya Ushirikiano mjini Paris, ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye utangazaji na utengenezaji wa vipindi kuhusu Michezo ya Olimpiki ya Paris.

Bw. Shen amesema, likiwa shirika kuu la utangazaji kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris ya mwaka 2024, CMG litatuma kikosi kazi chenye wataaluma zaidi ya elfu mbili kwenye michezo hiyo, na kutoa huduma za utangazaji za kiwango cha juu kwa kutumia teknolojia za kisasa za “5G+4K/8K+AI”.