Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, athari ya kuvuka mpaka ya mapigano yanayoendelea nchini Sudan yameathiri sana biashara kati ya nchi hiyo na Sudan Kusini, na pia kuongeza idadi ya raia wa Sudan Kusini wanaorejea nchini humo kutoka Sudan.
OCHA imesema mapigano hayo kati ya Jeshi la Sudan na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) yaliyoanza katikati ya mwezi April mwaka huu, yamepunguza uagizaji wa bidhaa kutoka, na hivyo kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula nchini Sudan Kusini.
Pia Ofisi hiyo imeripoti kuwa, watu 317,993 wameingia nchini Sudan Kusini kutoka Sudan tangu kuanza kwa mapigano hayo, na kuongeza kuwa, nusu ya watu hao ni wanawake, na nusu ya watoto ni wenye umri wa chini ya miaka 18.