Rais wa Congo azindua majengo mawili marefu yaliyojengwa na China
2023-10-24 10:28:17| cri

Rais wa Jamhuri ya Kongo Dennis Sassou Nguesso amezindua majengo mawili marefu yaliyojengwa wilayani Mpila, mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Brazzaville.

Waziri wa Miundombinu wa nchini humo amesema, majengo hayo yaliyojengwa na Kundi la Ujenzi na Uhandisi la Beijing (BCEG) la nchini China, ni alama ya nguvu ya maendeleo ya utalii.

Jengo litatumika kama kituo cha kibiashara, ambapo jengo moja litatumika kwa ajili ya ofisi, na lingine ni hoteli ya nyota tano.

Mradi huo uliohusisha mafundi wajenzi 800 kutoka Kongo na China, umefadhiliwa kwa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Kongo na Benki ya EXIM ya China.