CMG na Shirikisho la Tennis la Ufaransa wasaini hati ya kumbukumbu ya ushirikiano
2023-10-24 10:43:44| cri

Mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Shen Haixiong na mwenyekiti wa Shirikisho la Tennis la Ufaransa (FTT) Gilles Moretton jana Oktoba 23 walisaini hati ya kumbukumbu ya ushirikiano mjini Paris, ambapo wamekubaliana kushirikiana kwenye kueneza mchezo wa Tennis na kupanua ushirikiano kwenye utangazaji wa mashindano.

Bw. Shen Haixiong amesema, televisheni ya CCTV iliyo chini ya CMG, imetangaza mashindano ya tennis ya French Open tangu mwaka 1991, na kuhudumia watazamaji zaidi ya milioni mia moja kwa miaka mingi mfululizo. Bw. Shen ameeleza matumaini yake kuwa mchezo wa Tennis utakuwa daraja linalounganisha China na Ufaransa, kuhimiza mawasiliano ya kina kati ya watu wa pande hizo mbili.