Mkutano wa UM watoa wito wa kuzidi kushughulikia habari katika tume za kulinda amani
2023-10-24 09:43:13| CRI

Mkutano wa maandalizi kwa ajili ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2023 ulifanyika Jumatatu mjini Kigali nchini Rwanda, ambapo washiriki walisisitiza umuhimu wa kuimarisha mbinu za kukabiliana na changamoto za habari zilizomo ndani ya tume za kulinda amani.

Kwenye mkutano huo, Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Bw. Juvenal Marizamunda alisisitiza umuhimu wa mkutano huo, kwa kuwa tume za kulinda amani kote duniani zinakabiliwa na changamoto kwenye kazi za usambazaji askari. Alisema changamoto hizo zinaathiri zaidi kazi kuu ya kuwalinda raia ambapo habari feki, za uongo na kauli za chuki zinaenea kwa kasi zaidi kupitia vyombo vya habari vya kijamii.

Msaidizi wa katibu mkuu wa UM anayeshughulikia mambo ya Afrika Martha Ama Akyaa Pobee alitoa wito wa kuweka mkakati wa mawasiliano wa pande zote unaoendana na masuala makuu ya kisiasa na kiusalama.