Watu wanne wafariki kufuatia mafuriko ya ghafla nchini Somalia
2023-10-25 13:49:05| cri

Watu wanne wamefariki katika mafuriko ya ghafla yaliyotokea nchini Somalia.

Katika taarifa yake kuhusu hali ya Somalia iliyotolewa hivi karibuni, Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, watu watatu wamefariki katika wilaya ya Baidoa, kusini magharibi mwa Somalia, na binti wa miaka 13 amekufa maji katika kijiji kimoja mkoani Galmudug, katikati ya Somalia.

Kwa mujibu wa ripoti za awali zilizotolewa na wenza wake na wazee wa kaya katika wilaya ya Baidoa, watu karibu 122,000 wameathiriwa na mvua na mafuriko ya ghafla tangu Oktoba 4, wakiwemo wakimbizi wa ndani 92,000 wanaoishi katika makazi ya muda 178 wilayani humo.