Ripoti yaangazia uwezo wa ushirikiano wa kiviwanda kati ya China na Afrika
2023-10-25 10:12:51| CRI

Ripoti mpya iliyotolewa jana Jumanne mjini Beijing imeangazia uwezo wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuboresha mnyororo wa viwanda katika bara la Afrika.

Ripoti hiyo iliyopewa jina la "Uwekezaji wa China barani Afrika 2023," ilitayarishwa na kuchapishwa na Baraza la Biashara la China na Afrika na kukusanywa na baraza hilo, pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Biashara ya China na Afrika.

Ikiwa na kaulimbiu ya "Kuongeza thamani ya bidhaa za Afrika kwa kukuza maendeleo na mabadiliko ya minyororo ya viwanda barani Afrika," imejikita katika kupitia kesi 20 za makampuni ya China yanayowekeza barani Afrika. Inaangazia jukumu la makampuni ya biashara ya China katika maendeleo na mabadiliko ya minyororo ya sekta ya viwanda ya Afrika, na kubainisha uwezo wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika suala hili.

Afisa kutoka Wizara ya Biashara ya China Wang Dong, alisema China imesalia kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 14 mfululizo, na kuongeza kuwa China itashirikiana na Afrika kutekeleza miradi mikubwa ya ushirikiano kati ya China na Afrika na kuhakikisha mafanikio ya Baraza lijalo la Ushirikiano kati ya China na Afrika.