Watu 20 wauawa katika shambulio lililofanywa na kundi la ADF mashariki mwa DRC
2023-10-25 13:49:35| cri

Watu 20 wameuawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika shambulio linalotuhumiwa kufanywa na kundi la ADF lenye uhusiano na kundi la IS.

Shambulio hilo lilifanyika jumatatu usiku pembezoni mwa mji wa Oicha, katika eneo la Beni, mkoani Kivu Kaskazini.

Polisi wamesema, wapiganaji wa kundi la ADF pia wanahusika na mauaji ya wanadoa wawili waliokuwa kwenye fungate katika moja ya hifadhi za taifa za nchini Uganda yaliyotokea Oktoba 17.