Pande zinazopigana nchini Sudan zakubali kuhimiza kufikiwa kwa suluhu ya amani
2023-10-25 10:16:00| CRI

Serikali ya mpito ya Sudan inayoongozwa na Abdel Fattah Al-Burhan na vyama vya upinzani ambavyo vimetia saini Mkataba wa Amani wa Juba wa 2020 wamekubali kuhimiza kufikiwa kwa suluhu ya amani ya mzozo unaoendelea kati ya vikosi hasimu vya kijeshi.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa mashauriano uliofanyika mjini Juba, Sudan Kusini, naibu mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sudan Malik Agar alisema vita nchini Sudan vinaathiri kanda na Pembe ya Afrika, na kukomesha vita hivi kunategemea jinsi pande husika zinavyoweza kushughulikia masuala yao ya ndani kwa kujadili njia za kuyatatua.

Alishutumu baadhi ya nchi kwa kuchochea mapigano kati ya jeshi la Sudan linaloongozwa na Al-Burhan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ili kuteka baadhi ya maeneo ya Sudan.