Misri yatangaza duru mpya ya mazungumzo ya pande tatu kuhusu Bwawa la GERD
2023-10-25 22:49:59| cri

Wizara ya Rasilimali ya Maji na Umwagiliaji ya nchini Misri imesema, duru mpya ya majadiliano ya ngazi ya mawaziri kuhusu Bwawa la GERD imeanza jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa nchi hiyo, Misri, na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Misri, Sudan na Ethiopia.

Wizara hiyo pia imesema, awamu hii ya mazungumzo ni mwendelezo wa mchakato wa mazungumzo unaoendelea, ambapo ndani ya miezi miwili, awamu mbili za mazungumzo hayo zilifanyika mjini Cairo, na baadaye mjini Addis Ababa, Ethiopia.