IMF yasema China si chanzo cha mzigo wa madeni kwa nchi za Afrika kusini mwa Sahara
2023-10-26 10:19:06| cri

Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imesema, China si chanzo cha changamoto za madeni yanayozikabili nchi za Afrika kusini mwa Sahara, ingawa mikopo yake katika bara hilo imesaidia ukuaji wa nchi za Afrika kusini mwa Sahara katika miongo miwili iliyopita.

Ripoti hiyo iliyotolewa mwezi uliopita imesema, China, ikiwa ni mkopeshaji mkubwa wa pande mbili katika kanda hiyo, deni lake la nje liliongezeka kwa asilimia chini ya 2 kabla ya mwaka 2005 na kufikia asilimia 17 mwaka 2021, ambayo ni sawa na dola za Marekani bilioni 790.

Ripoti hiyo ya IMF inaelekea kupinga tuhuma za nchi za Magharibi kuwa ongezeko la mikopo inayotolewa na China kwa nchi za Afrika ni chanzo kikuu cha mzigo wa madeni kwa nchi hizo, kauli ambayo inaungwa mkono na maofisa wa serikali za Afrika.