Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vimetangaza kuwa wajumbe wao wamewasili katika mji wa bandari wa Jeddah nchini Saudi Arabia ili kuanza tena duru mpya ya mazungumzo.
Jeshi la Sudan limesema kwenye taarifa kuwa linaamini mazungumzo ni njia mojawapo ya kuweza kumaliza vita hivyo, wamekubali mwaliko wa kwenda Jeddah kukamilisha yale ambayo yalikubaliwa awali ambayo ni utekelezaji kamili wa Azimio la Jeddah ili kuhakikisha kazi za kibinadamu na watu wa kawaida wanarudi katika miji ambayo waasi walifanya uharibifu mkubwa wa uporaji, kuchoma moto, kulipua mabomu na kubaka watu kiholela, lakini jeshi hilo limesisitiza kwamba kuanza tena kwa mazungumzo hakumaanishi kusitishwa kwa makabiliano ya silaha dhidi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF.
RSF, kwa upande wake, ilieleza matumaini yao kwenye taarifa kuwa jeshi la Sudan linaweza kuonyesha uaminifu, uhalisia, na nia ya kufikia suluhu ambapo litasimamisha vita na kumaliza mateso ya watu.