Serikali ya Uganda yatoa fursa ya kuwasamehe waasi wa kundi la ADF
2023-10-26 09:57:15| CRI

Serikali ya Uganda Jumatano ilitangaza kuwasamehe waasi wa kundi la ADF endapo wataacha shughuli za uasi dhidi ya serikali.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa serikali ya Uganda ambaye pia ni waziri wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa nchi hiyo Chris Baryomunsi, ambapo ameongeza kuwa serikali ya Uganda imetoa nafasi ya kuwasamehe wale walioandikishwa na kundi la ADF na kutaka kujisalimisha na kuacha mapambano dhidi ya watu wa Uganda wasio na hatia. Wakiomba kusahemewa na kujitoa kwenye kundi la ADF, watasahemewa kwa mujibu wa sheria. Lakini hakueleza ni wakati gani.