Maonyesho maalumu ya “Safari kupitia ustaarabu tofauti” ya CMG yafunguliwa kwenye Palace of Nations
2023-10-27 10:07:54| CRI

Maonyesho malumu ya “Safari kupitia Ustaarabu Tofauti” yanayoandaliwa kwa pamoja na Shirika kuu la Utangazaji la China CMG, ofisi ya China katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva na ujumbe wa China katika mashirika mengine nchini Uswizi yamefunguliwa jana tarehe 26 huko katika Kasri ya makabila(Palace of Nations).

Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong amehutubia kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo akisema, maonyeshao hayo yanatumia uvumbuzi wa teknolojia ya kidijitali, kuwaongoza watembeaji wa nchi za nje kuelewa chanzo cha ustaarabu wa China wenye historia ya miaka karibu elfu 5, na kujionea vivutio maalumu vya ustaarabu wa China.

Mwenyekiti wa kamati ya utamaduni wa ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Francesco Pisano amesema, anatarajia maonyesho hayo yataleta historia na ustaarabu wa China kwenye nchi za magharibi, ili watu waweze kuwa na uzoefu wa utamaduni anuai wa China, na kufanya kazi za vyombo vya habari kwa ajili ya kuhimiza mawasiliano kati ya ustaarabu tofauti.