Baraza Kuu la UM laendelea na kikao cha dharura kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina
2023-10-27 10:20:37| cri

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeendelea na kikao chake cha 10 cha dharura kuhusu mgogoro kati ya Israel na Palestina.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho, Rais wa Baraza hilo, Dennis Francis amelishutumu kundi la Hamas kwa shambulio lake dhidi ya Israel Oktoba 7, na kuituhumu Israel kwa mashambulio yake yanayolenga raia na kuharibu miundombinu muhimu katika Ukanda wa Gaza.

Amesema pande zote zinapaswa kuzingatia sheria ya kibinadamu ya kimataifa na kuweka mazingira muhimu ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikishwa kwa wahitaji katika Ukanda wa Gaza. Amesema njia pekee ya amani ya kudumu katika eneo hilo ni majadiliano ya suluhisho la nchi mbili, kuendana na sheria ya kimataifa, Mkataba wa Umoja wa Mataifa na maazimio husika ya Umoja huo.