Serikali ya Somalia yapitisha muswada wa kupambana na uhalifu wa baharini
2023-10-27 23:21:13| cri

Serikali ya Somalia imepitisha sheria inayolenga kuimarisha juhudi za kukabiliana na uhalifu wa baharini ikiwemo uharamia na utekaji nyara, lengo likiwa ni kuhakikisha usalama wa pwani ya nchi hiyo kwa shughuli za kiuchumi.

Muswada wa kupambana na uharamia na utekaji nyara, unaoeleza adhabu kali kwa watu wanajihusisha na uhalifu wa baharini, uliwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri na Waziri wa Sheria na Katiba wa nchi hiyo, Hassan Moalim Mohamud. Amesema mfumo mpya wa sheria utaongeza nguvu ya hatua za kupambana na uharamia na utekaji nyara katika bahari ya Hindi na maeneo mengine ya kimataifa baharini, na kuwa hatua kubwa katika kukabiliana na uharamia na kuhakikisha mchakato wa wazi na usawa wa kisheria kwa watuhumiwa.

Muswada huo utapelekwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa.