Waziri Mkuu wa Ethiopia arejea ahadi ya nchi hiyo katika operesheni za ulinzi wa amani duniani
2023-10-27 10:29:47| cri

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed jana alhamis amerejea tena ahadi ya nchi hiyo katika operesheni za kulinda amani duniani.

Bw. Abiy amesema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Jeshi la nchi hiyo. Amesema Ethiopia itaendelea kupeleka askari wa kulinda amani duniani kama sehemu ya wajibu wake wa kimataifa, na kutoa wito kwa jeshi la nchi hiyo kuwa tayari siku zote kuhudumia, sio Ethiopia pekee, bali bara la Afrika na dunia nzima pale inapohitajika.

Kwa sasa, Ethiopia ni moja ya nchi zinazopeleka askari wengi wa kulinda amani katika majukumu ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.