Juhudi za wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi
2023-11-17 08:00:26| CRI

Kuna kauli maarufu sana hapa nchini China ambayo inaelezea ujasiri na juhudi za wanawake ainayosema,"Wanawake ni nusu ya anga". Kauli hii ni sahihi kabisa hasa tunaposhuhudia juhudi za wanawake katika ngazi mbalimbali kuanzia familia, jamii hata ngazi ya taifa. Hivi majuzi tu Kongamano la 13 la wanawake wa China lilifanyika hapa mjini Beijing na kuangazia mchango mkubwa wa wanawake wa China tangu Mkutano wa 12 wa Taifa wa Wanawake.

Katika miaka ya hivi karibuni, mamia ya mamilioni ya wanawake nchini China wamefanya kazi kwa bidii katika vita vya kupambana na umaskini, ambapo historia inatuambia kuwa wanawake, ambao ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu, ni nguvu kubwa ya kukuza maendeleo ya jamii nzima nchini China. Ushindi wa kila shughuli unahusisha kazi ngumu ya wanawake. Hivyo leo hii tutatapa ripoti kuhusu mkutano huu wa wanawake wa China, na pia baadaye tutaangalia historia na maisha ya kiongozi maarufu mwanamke nchini Tanzania ambaye hivi majuzi tu alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Jokate Mwegelo.