Baadhi ya wake wa marais huwa ni watu wenye ushawishi mkubwa hasa pale wanapochukua jitihada katika kuhakikisha wanasaidia ustawi wa jamii kwenye nyanja mbalimbali. Baadhi yao huwa wanasiasa na wanaharakati ambao huchukua jukumu katika safari za kisiasa na kusaidia serikali zinazoongozwa na wenza wao.
Hivyo leo kwenye kipindi cha ukumbi wa wanawake tutaangalia wanawake wanaojitoa kuhamasisha wengine akiwemo Mama Janeatte Nyiramongi, ambaye wengi wao kwa sasa wanamtambua kama Jeannette Kagame, ambaye ni mke wa rais wa Rwandwa, Paul Kagame, Jeannette Kagame ni mwanamke mwenye rangi halisi ya kiafrika mwenye umbile kubwa na mrefu wa kimo, ukiachilia hayo ambayo yanaonekana, lakini Janeatte Nyiramongi Kagame, ni nani hasa? Na amekuwa na mchango gani katika mafanikio ya rais Kagame? Na pia tutamwangalia Mganda anayeishi hapa nchini China na kujibebea umaarufu kwenye mtandao wa tiktok.