Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC yafanya mkutano kujadili sera na hatua za kustawisha sehemu ya Kaskazini Mashariki
2023-10-29 18:33:12| CRI

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano uliojadili maoni juu ya sera na hatua za kuendeleza kwa pande zote sehemu ya kaskazini mashariki mwa China katika zama mpya.

Mkutano huo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, Xi Jinping, umeeleza kuwa kuhimiza ustawishaji wa sehemu hiyo ni uamuzi muhimu wa kimkakati uliowekwa na Kamati Kuu ya CPC.

Pia umesisitiza kuwa, ni muhimu kushikilia kithabiti jukumu kuu la kuhimiza maendeleo yenye sifa bora, na kazi ya kimkakati ya kujenga muundo mpya wa maendeleo, kuratibu maendeleo na usalama, na kuimarisha umuhimu wa kimkakati wa sehemu ya kaskazini kashariki.

Mkutano huo pia umeutaka uongozi wa Chama utekelezwe katika mchakato mzima wa kuhimiza ustawishaji wa sehemu ya kaskazini mashariki mwa China katika zama mpya, kuimarisha mapambano dhidi ya ufisadi, na kuboresha mazingira ya kisiasa, ili kuhamasisha imani ya maendeleo.