CMG yaanzisha ushirikiano na Kituo cha maingiliano ya ustaarabu kati ya China na Ugiriki na Chuo cha Olimpiki cha Kimataifa
2023-10-29 20:23:40| CRI

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limesaini mikataba ya ushirikiano na Kituo cha maingiliano ya ustaarabu kati ya China na Ugiriki na Chuo cha Olimpiki cha Kimataifa, ili kukuza maingiliano ya ustaarabu kati ya China na Ugiriki na moyo wa Olimpiki.

Mkurugenzi wa CMG Shen Haixiong kwa nyakati tofauti amesaini mikataba na mwenyekiti wa Baraza la Kituo cha maingiliano ya ustaarabu kati ya China na Ugiriki Stelios Virvidakis, na mkuu wa Chuo cha Olimpiki cha Kimataifa Isidoros Kouvelos.

Waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis na serikali ya Ugiriki, kupitia naibu waziri wa Michezo Yannis Vroutsis, wamepongeza ushirikiano mpya kati ya Chuo cha Olimpiki cha Kimataifa na CMG, na kutumai kuwa thamani ya Olimpiki itakuzwa nchini China.