Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya treni nchini India yafikia 6
2023-10-30 08:34:03| cri

Watu sita wamefariki na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea katika jimbo la Andhra Pradesh kusini mwa India Jumapili jioni.

Waziri Mkuu wa India Bw. Narendra Modi amesema mamlaka nchini humo zinatoa usaidizi unaowezekana kwa waathiriwa, pia ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa, na kuwapa pole majeruhi.

Ajali hiyo ilitokea wakati treni ya abiria ya Visakhapatnam-Rayagada ilipogongana na treni nyingine ya abiria ya Visakhapatnam-Palasa na kusababisha mabehewa matatu ya treni ya Visakhapatnam-Rayagada kutoka kwenye njia yake.