Israel yaongeza mashambulio ya ardhini katika Ukanda wa Gaza
2023-10-30 08:34:08| CRI

Israel imeongeza mashambulio ya ardhini katika Ukanda wa Gaza na kuongeza mashambulio ya anga katika eneo hilo lililozingirwa huku idadi ya watu waliouawa katika Ukanda wa Gaza ikifikia 8,005.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel Daniel Hagari amesema, jeshi hilo limeongeza askari wake wanaoingia kwenye Ukanda wa Gaza, na kuongeza kuwa, operesheni za sasa za ardhini zinalenga zaidi sehemu ya kaskazini ya Ukanda wa Gaza.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant jana jumapili alikutana na wawakilishi wa familia za watu 230 waliotekwa nyara na kundi la Hamas katika shambulio la tarehe 7 mwezi huu dhidi ya Israel, na kusema kuwa, mashambulio ya ardhini ni sehemu ya juhudi za kuwaokoa mateka hao.