Rais wa Kenya William Ruto Jumamosi iliyopita amesema, nchi hiyo itaondoa mahitaji ya visa kwa Waafrika wote itakapofika mwisho wa mwaka 2023, ili kuhimiza biashara na nchi za Afrika.
Akizungumza kwenye mkutano wa kilele wa Mabonde Matatu uliofanyika huko Brazzaville nchini Jamhuri ya Congo, Rais Ruto amesema, hadi kufikia mwisho wa mwaka huu, hakuna mwafrika atakayehitaji visa kuingia nchini Kenya, na wakati wa kutambua umuhimu wa kufanya biashara kati ya nchi za Afrika umefika.
Rais Ruto pia alizungumzia kiwango cha chini cha biashara ya ndani kati ya nchi za Afrika, na kutoa wito wa kupunguza ushuru wa forodha ndani ya bara hilo ili kuharakisha utekelezaji wa eneo la biashara huria barani humo.