AU yatoa wito kwa uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake ili kumaliza uhalifu wa kijinsia
2023-10-30 08:35:27| CRI

Umoja wa Afrika umetoa msisitizo katika haja ya kuimarisha juhudi za kina na kuongeza uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake ili kumaliza mzunguko wa uhalifu dhidi ya wanawake na wasichana barani Afrika.

Katika taarifa yake iliyotolewa hivi karibuni, Umoja wa Afrika umesema uwezeshaji wa kifedha ni sehemu muhimu ya kutimiza usawa wa kijinsia, kuwawezesha wanawake, na kukabiliana na ongezeko la uhalifu wa majumbani. Umoja huo umesema uhalifu dhidi ya wanawake na wasichana ni ukiukaji wa haki ya msingi ya binadamu, suala linalohatarisha afya ya jamii, na wenye madhara makubwa kwa ustawi wa binadamu.

Wito huo umetolewa kabla ya mkutano wa uwezeshaji wa wanawake unaoandaliwa na Umoja huo, uliopangwa kuanza leo Oktoba 30 hadi kesho katika mji mkuu wa Visiwa vya Comoro, Moroni.