Wanafunzi wampiga mwalimu mkuu 'kwa kuwapa uji usio na sukari'
2023-10-31 14:22:14| cri

Maofisa wa elimu katika eneo la Homa Bay nchini Kenya wanafanya uchunguzi kuhusu tukio la Mkuu wa shule ya sekondari kushambuliwa na wanafunzi baada ya kutuhumiwa kuwapa wanafunzi hao uji usio na sukari.

Tukio hilo lilitokea Ijumaa asubuhi wakati mwalimu wa shule moja ya sekondari kukutwa na majeraha mwilini baada ya wanafunzi kumvamia kwa madai ya kusimamia vibaya shule hiyo. Ripoti ya polisi iliyowasilishwa na uongozi wa shule, imesema mkuu huyo wa shule alikuwa nyumbani, na alivamiwa baada kukataa dai la wanafunzi wa vidato mbalimbali waliomfuata nyumbani na kutaka kuandamana naye kituo cha polisi cha eneo hilo.

Mashuhuda wamesema wanafunzi hao waliokuwa na hasira walimpiga mwalimu huyo, lakini baadaye aliokolewa na polisi. Mwenyekiti wa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari nchini Kenya mjini Suba, Bw Paul Mbara, amelaani shambulizi hilo.