Idadi ya watalii waliofika Zanzibar yazidi milioni moja
2023-10-31 14:23:17| cri

Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar imesema idadi ya watalii waliotembelea kisiwa hicho imeongezeka kwa asilimia 110.28 kutoka 260,644 wa mwaka 2020 hadi 548,503 mwaka 2022, Idadi hiyo ni watalii wa kimataifa, na idadi hiyo ikijumuishwa na watalii wa ndani imefikia kiwango cha juu cha milioni moja (1,000,000), ambacho kiliwekwa na mamlaka kufikiwa ifikapo 2025.

Waziri wa Utalii na Urithi wa Zanzibar Bw. Simai Mohammed Said, amethibitisha kuwa idadi ya watalii imekaribia kufikia milioni moja.

Licha ya changamoto zilizotokana na janga la Covid-19, miaka michache iliyopita imeshuhudia mabadiliko kamili kwenye sekta ya utalii.