UNITAMS yakaribisha pande mbili za mgogoro wa Sudan kurejesha mazungumzo ya amani
2023-10-31 23:15:12| cri

Tume ya msaada ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNITAMS imekaribisha wajumbe wa jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kufanya mazungumzo ya amani huko Jeddah nchini Saudi Arabia.

Tume hiyo imeeleza kuwa, inatumai duru mpya ya mazungumzo itawezesha pande mbili kufuata ahadi ya kulinda raia wa Sudan iliyosainiwa mwezi Mei mwaka 2023, na kutimiza usimamishaji vita kwa pande zote.

Tume hiyo pia imesisitiza kuwa, itaendelea kushirikiana na mashirika ya kimataifa na kikanda ikiwemo Umoja wa Afrika, IGAD kuunga mkono juhudi za usuluhishi, ili kutatua mgogoro wa Sudan kwa njia ya amani.