Mgogoro unaoendelea Mashariki mwa DRC watishia usafirishaji wa msaada wa kibinadamu
2023-10-31 08:24:02| cri


 

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric jana amesema, mgogoro uliotokea hivi karibuni kati ya jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na vikosi vya waasi unatishia usafirishaji wa msaada wa kibinadamu.

Bw. Dujarric amesema, Tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRC ina wasiwasi kuhusu mapigano yanayotokea kila siku mkoani Kivu Kaskazini kati ya wapiganaji wa kundi la M23, na jeshi la DRC na muungano wa makundi yenye silaha tangu mwanzo wa mwezi huu.

Bw. Dujarric amesema mgogoro huo ulitishia sana operesheni za kupeleka misaada ya kibinadamu katika maeneo wanayoishi wakimbizi wa ndani katika mji wa Goma.