Tume ya haki za binadamu ya nchini Ethiopia yatoa wito wa suluhisho la amani kaskazini mwa nchi hiyo
2023-10-31 08:25:29| CRI

Tume ya Haki za Binadamu ya nchini Ethiopia (EHRC) imetoa wito wa suluhisho la amani la mapigano yanayoendelea katika mkoa wa Amhara, kaskazini mwa nchi hiyo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, Tume hiyo imesema kipaumbele kinapaswa kutolewa kwa suluhisho endelevu la mgogoro nchini humo, ambako katika miezi ya karibuni, mapigano makali kati ya vikosi vya usalama vya Ethiopia na wapiganaji wa kundi la Kano yamesababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kupoteza makazi yao.

Taarifa hiyo pia imezitaka pande zinazopigana kuhakikisha haki za watu waliokamatwa, na pia kuhakikisha wajibikaji katika matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwemo kesi za ubakaji na mauaji.

Mwezi Agosti, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa iliripoti kuwa, mapigano katika mkoa wa Amhara yamesababisha vifo vya watu 183 tangu mwezi Julai mwaka huu.